# NJIIMNET — The car network

> The car network (iPhone/iPad app by Olorok Enterprises Limited.)

- Source: https://appshunter.io/ios/app/njiimnet/id6740287568 (this page in markdown: same URL + `.md`)
- Developer: [Olorok Enterprises Limited](https://appshunter.io/developer/1687318463)
- Category: Shopping
- Price: Free
- Age rating: 4+
- Requires: iOS 15 · 54 MB
- Languages: American English
- Released: 2025-07-15
- Data updated: 2026-08-20
- User reviews in markdown: https://appshunter.io/ios/app/njiimnet/id6740287568/reviews.md

## What is NJIIMNET?

Kwa miaka mingi, kununua au kuuza gari kumekuwa na changamoto. Bei zisizo wazi, ada zisizotarajiwa, na maamuzi makubwa bila taarifa kamili. Tumekutengenezea njia rahisi zaidi.

Kama unataka kununua au kuagiza gari, NJIIMNET inakusaidia ku-:
- Jua bei halisi ya gari kuendana na mwenendo wa soko
- Nunua kwa bei ya haki
- Okoa muda & nguvu
- Pokea ofa nyingi kutoka kwa wauzaji
- Linganisha bei kirahisi
- Kwepa kulipa zaidi

Kama muuzaji, NJIIMNET inakusaidia ku-:
- Pata wateja wenye uhitaji
- Uza bila kufanya matangazo
- Fikia mteja sahihi katika muda muafaka
- Jua bajeti ya wateja kabla hata hujaongea nao
- Pata wateja bure
- Chagua ulipe kamisheni au la
- Lipia kamisheni utakapouza gari tu
- Uza haraka zaidi
- Pata taarifa za muhimu za wateja kabla ya kulipia chochote

NJIIMNET unganisha moja kwa moja na wanunuzi na wauzaji wa magari, huku ikihakikisha uwazi na kurahisisha mchakato mzima.


## Version history (last 5 releases)

### 5.6.4 — 2026-08-11

Tunajali mazingira. Tunajali kizazi cha kesho.

Jukumu la kutunza na kuhifadhi mazingira ni letu sote. Tunawashukuru kwa kuungana nasi katika safari yetu ya kufanya soko letu la magari kuwa na ufanisi bora, lenye ukweli na uwazi, na linalozingatia utunzaji wa mazingira.

Sasa unaweza kuona gari inatoa hewa chafu (CO2e) kiasi gani, kwa kilomita moja na kwa safari zako za mwezi mzima. Hii ni kwa ajili ya kukusaidia kufahamu magari yenye utendaji kazi wa juu na ambayo ni mazuri kwa mazingira.

### 5.6.3 — 2026-06-27

Tunajali mazingira. Tunajali kizazi cha kesho.

Kila tunachofanya NJIIMNET, tunaamini katika kuinua Afrika yetu. Kwa kukusaidia kujua ni brand gani zina magari ya umeme na hybrid, tunachangia katika kutunza na kuhifadhi mazingira yetu kwa pamoja.

### 5.6.2 — 2026-06-14

Tunajali mazingira. Tunajali kizazi cha kesho.

Jukumu la kutunza na kuhifadhi mazingira ni letu sote. Tunawashukuru kwa kuungana nasi katika safari yetu ya kufanya soko letu la magari kuwa na ufanisi bora, lenye ukweli na uwazi, na linalozingatia utunzaji wa mazingira.

### 5.6.1 — 2026-06-07

GHARAMA ZA KUMILIKI GARI

Tulianza kwa kurahisisha kujua bei ya gari kuendana na mwenendo wa soko.

Kisha tukakuwezesha kufahamu gharama za kuendesha gari kutokana na matumizi yake ya mafuta.

Kisha tukakuwezesha kufahamu gari la umeme linatumia umeme kiasi gani, full battery itakusafirisha umbali gani, na itakugharimu shilingi ngapi kuliendesha mwezi mzima.

Sasa, unaweza kufahamu jumla ya gharama za mafuta kwa miaka unayotarajia kulimiliki.

Pata yote haya bure kwa kutumia NJIIMNET sasa.

### 5.6.0 — 2026-06-02

MAGARI YA UMEME (EVs)

Tulianza kwa kurahisisha kujua bei ya gari unalotaka kuendana na mwenendo wa soko ili kukusaidia kupata gari sahihi kwa bei sahihi.

Kisha tukakuwezesha kufahamu gharama za kuendesha gari kutokana na matumizi yake ya mafuta.

Sasa, unaweza kufahamu gari la umeme (EV) linatumia umeme kiasi gani kutembea kilomita moja, full battery itakusafirisha umbali gani (range), na itakugharimu shilingi ngapi kuliendesha mwezi mzima.

Pata yote haya bure kwa kutumia NJIIMNET sasa.

## Apps similar to NJIIMNET

| App | Rating | Price | Category |
| --- | --- | --- | --- |
| [GariPesa – Buy & Sell Cars Tz](https://appshunter.io/ios/app/garipesa-buy-and-sell-cars-tz/id6747010706) | — | Free | Shopping |
| [Dar Shopping: E-Marketplace](https://appshunter.io/ios/app/dar-shopping-e-marketplace/id1666150951) | — | Free | Shopping |
| [Mkinga Empire](https://appshunter.io/ios/app/mkinga-empire/id6740182264) | — | Free | Shopping |
| [Tunzaa](https://appshunter.io/ios/app/tunzaa/id1578263762) | 5.0 (3) | Free | Shopping |
| [Uhuru Market](https://appshunter.io/ios/app/uhuru-market/id6702008464) | — | Free | Shopping |
| [Nida & Danish](https://appshunter.io/ios/app/nida-and-danish/id6443723159) | 5.0 (1) | Free | Shopping |

## More apps by Olorok Enterprises Limited

- [Ng'ongo](https://appshunter.io/ios/app/ngongo/id6448993793)

All apps by Olorok Enterprises Limited: https://appshunter.io/developer/1687318463

## Related topics

[garoon](https://appshunter.io/ios/topics/garoon) · [bushi navi](https://appshunter.io/ios/topics/bushi-navi) · [imikimi zo](https://appshunter.io/ios/topics/imikimi-zo)

---

*Data collected daily from the US App Store and indexed by [AppsHunter](https://appshunter.io/). User reviews are verbatim App Store reviews. Ratings, prices and chart positions refresh continuously; this snapshot is from 2026-08-20.*
