
Msafiri Plus
Kata tiketi popote, na offline
0 ratings
Free
About
Msafiri Plus ni app ya wakala wa mabasi. Kata na uza tiketi za safari popote ulipo — mtaani, kituoni au ndani ya basi — hata bila mtandao. Imejengwa kwa ajili ya mawakala, vituo na kampuni za mabasi Tanzania.
KWA NINI MSAFIRI PLUS
• Uza popote, hata offline — Endelea kuuza tiketi bila mtandao; taarifa husawazishwa zikirudi mtandaoni.
• Chapisha papo hapo — Unganisha printa ya thermal na umpe abiria tiketi kamili kwa sekunde.
• Ratiba za kampuni zote — Safari zote za siku, nauli, namba za magari na siti zilizobaki mahali pamoja.
• Chagua siti moja kwa moja — Ramani ya siti inayoonyesha zilizouzwa na zilizo wazi kwa wakati halisi.
• Zuia udanganyifu — Kila tiketi ina QR ya kipekee; skani kuhakiki, na tiketi iliyotumika haiwezi kutumika tena.
• Simamia salio lako — Ongeza floti na uone matumizi kwa uwazi.
• Ripoti za kila siku — Mauzo, idadi ya tiketi, abiria na komisheni yako kwa muhtasari wa haraka.
• Ada ya kujiunga: BURE — Anza kuuza leo bila gharama ya awali.
Jiunge na mtandao unaokua wa mawakala wa Msafiri Plus. Kwa usaidizi, tupigie 0755 277 133.
Imetengenezwa na LOGIX.
Show more
What's New in Msafiri Plus
1.0.25
August 16, 2026
Performance improvement





